patanisho

PATANISHO: Mjomba wangu alinipiga kwa chuma kichwani

Collins, 23, kutoka Narok ndiye aliyeomba kupatanishwa na mjombake, bwana Peter, 47, akidai kuwa wawili hao walikosana na hadi akapigwa chuma cha kichwa na kumlaani. Aliongeza kuwa mjombake ndiye mzazi wake na sahii anasononeka na anafikiri kujitoa uhai.

“Nilikuwa na mwanadada mpenzi wangu nikiwa naishi kwa yule mjomba, niliondoka na kwenda Nairobi kutafuta kazi ila sikupata na nikateseka. Nilikuwa nimefungua kinyozi na mjomba wangu wakapangana na mwanadada wakauza zile mashini na akaenda kwao.” Alielezea.

PATANISHO: Mume wangu aliniambia nitaendea kifo krisimasi

Collins anadai mjomba hakuuza mashini zote ila alipoenda kuidai wakaanza vita na kwa mwaka mzima hajasafiri hadi nyumbani. Juzi alitishiwa kuwa asiwahi fika kwa shamba la ukoo wao.

Ni mchungaji pia na ndiye amekuwa akinilea kwa mambo ya kiroho.” Aliongeza.

Alipopigiwa simu bwana Peter alisema kuwa alimlea Collins maisha yake na kijana amekuwa akimkosea na kumtumia arafa za matusi.

“Najua ni mtoto mdogo na sote tunahitaji msaada kutoka kila mmoja, juzi alikuja nyumbani akitaka kunichapa na hata kama nilikosea angekuja tuzungumze vyema, hadi nikaapa kuwa hatakanyanga hapa.” Alieleza bwana Peter.

PATANISHO: Nashuku boss wangu mwanajeshi ana uhusiano na mke wangu

Akijitetea, Collins alisema kuwa chanzo chake cha kumtumia ujumbe ni kuwa mjombake alikuwa amesema kuwa asiwahi patikana kwa shamba la nyanya. Hapo akaamua kumpigia simu na kumueleza kuwa angemwambia yeye mwenyewe.

Nilipofika kule kwa mjomba alikuwa amebeba panga na kama sio ndugu angeniua na isitoshe alitoa chuma kotini mwake na ikaniumiza hadi nikkashonwa hospitalini.”

Mjombake alimaliza akisema kuwa arafa hizo zote ziko kwa polisi kwani alihatarisha maisha yake kwa njia kubwa. Alisema amemsamehe lakini aite jamii ili aombe msamaha na aape kuwa hatorudia tena.

 

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments