PATANISHO: Mke wangu alimwagia nguo zangu maji ili nisiende mahali

Mama Shedi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe ambaye walikosana tarehe tatu mwezi wa tano mwaka huu na akabeba nguo zake zote na kuondoka na hajui aliko. Anaomba asaidiwe ili ndoa yao ya miaka saba iokolewe.

"Alilala nje akija nikampigia kelele ile kawaida akaendelea hivo akaanza kufika saa tano ama saa sita, siku moja nikamtusi kwani nikimuongelesha alikuwa ananyamaza. Hapo alikasirika na kuondoka akisema hajawahi tusiwa na mwanamke." Alielezea akisisitiza kuwa mumewe anampenda lakini shida ni ya kufika nyumbani akiwa amechelewa.

Wawili hao ambao wamejaliwa watoto wawili huzungumza lakini bado mumewe hajarudi nyumbani.

"Si nilikuambia nimekusamehe?" Aliuliza baba Shedi kabla ya kukatiza mawasiliano kati yetu.

Kulikuwa na dem nashuku alikuwa naye lakini hataki kuskia story zake. Aliongeza mama Shedi.

Tulikosana, kuna mahali kulikuwa na function ya rafiki yangu na mdosi ndio alikuwa anaenda lakini kwa sababu hakuwa anahisi vizuri akaniambia niende kwa niaba yake.

Asubuhi nikitoa mavazi yangu, mke wangu akanimwagia maji baridi. Nikatoa mengine na akanimwagia tena, nilipotoa zingine zote akaziweka kwa beseni ili nisiende mahali.

Wakati niliona tunasumbuana naye nikanunua nguo zingine na kufika kazini akaleta mtoto hapo lakini hakunipata.

Aliongeza akisema kuwa yeye ni shabiki wa kadanda na kwa kuwa kuna mechi za Champions League yeye hurudi akiwa amechelewa na mkewe hushuku kuwa ana mipango ya kando.

Licha ya hayo yote alisema kuwa atarudi nyumbani leo.