PATANISHO: Mke wangu alinichota kila kitu na kuniwachia mulika mwizi

patanisho.
patanisho.
Bwana Wycliffe alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Agnes, ambaye walikosana na kubeba vitu vyote kwa nyumba na kumuacha mpweke.
"Mke wangu alianza kuskiza mambo ya jirani eti nina wanawake wengine na kila nikipigia mtu simu yeye hudai kuwa nazungumza na wanadada wengine.

Siku moja nilipoelekea kazini nilipata amebeba kila kitu kwa nyumba na sasa nateseka." Alielezea Wycliffe.

Wycliffe ambaye anafanya kazi ya useremala anadai kuwa yeye huzungumza na wateja hadi usiku na hilo lilipelekea wawili hao kubishana.

Anadai kuwa juhudi zake za kurudiana na mkewe hazijawahi fua dafu licha yake kumtumia nauli ili arudi.

"Tulianza naye chini na tukanunua kila kitu nyumbani na sasa alibeba kila kitu na kuniachia tu kitanda na kitu, isitoshe alichukua hadi simu yangu na kuniwachia mulika mwizi." Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili unusu lakini bado hawajajaliwa na mtoto.

Alipopigiwa simu bi Agnes, alisema ulevi wa mumewe ndio unamkasirisha kwani yeye hulewa hadi akiwa kwa nyumba.

Wycliffe naye alijitetea akisema kuwa akiwacha pombe kwa mwezi mmoja mkewe humuuliza mbona amekawia bila kulewa na akilewa tena huwa shida.

"Hatujaishi naye miaka mitano ila miaka miwili na nusu." Alisema Agnes.