PATANISHO: Mke wangu alisema amepata jamaa mwenye fedha kuniliko

Odhiambo, 28, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Jacqueline, 26, baada ya kumpiga na mkewe kukusanya virago vyake na kuondoka.

"Najua nilikosa na na regret sahii. Ilifanyika last week on Wednesday.

Mke wangu hutokea kazi usiku sana na hiyo siku nilipata mtoto kwa nyumba akilia, nilipompigia simu kumuuliza kama haji akasema haji na akanipigia mdomo.

Nikampigia mara tano huku akikata, aliporudi nikamuuliza mbona hakusema alipokuwa na akaniuliza kama alikuwa amebeba sufuria, hapo nikakasirika na nikamzaba kofi." Alisimulia Odhiambo.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa mtoto mmoja.

Nilifanya uchunguzi na mahali yupo yuaishi na jamaa mwingine ambaye alisema kuwa ana fedha zaidi kuniliko.

Alipopigiwa simu bi Jacqueline, alifichua kuwa kuna maneno mengi ambayo mumewe amemtendea na kuwa hana haja ya kuyazungumzia hewani.

"Kuna time yenye nilikuwa nimefungua shop mahali na nikawacha juu ya huyu. Alikuwa anavunja simu yangu daily na ikabidi niwache ile job basi." Alisema Jacqueline.

Hata nywele amekuwa aking'oa hata ukaona kichwa changu waweza piga nduru." Alisisitiza akisema kuwa mumewe alikuwa anapenda waganga.

Akijitetea Odhiambo alisema hakuwahi tumia fedha kupitia uganga na kuwa kama angeweza sahii angekuwa billionaire.