PATANISHO: Mke wangu ana tabia ya kunitusi kila uchao

patanisho
patanisho
Bwana John 32, aliomba apatanishwe huku akidai ndoa yake imeharibika akisema mkewe, bi Hellen, 26, anamtusi mchana kutwa, usiku kucha na isitoshe amesema mkewe amefanya wakosane na shemejiye licha yake kupenda mke wake na familia yake.

"Napitia masaibu kwani nimeoa kwa miaka sita na nimekuwa na changamoto nyingi. Mara mimi nahusika na mipango ya kando na tunasuluhisha lakini tunasuluhisha kabla ya shida nyingi ziibuke." Alisema John.

Aliongeza,

Hii shida ilianza nilipofunga ndoa kwani nilikuwa na mpenzi kabla ya kumuoa mke wangu, tukaketi kama familia na tukasuluhisha na maisha ikaendelea."

John anasema kuwa tangia aamue kutulia kwa ndoa amekuwa na mpango wa kando miaka miwili iliyopita lakini wamekuwa wakipigana mara kwa mara.

"Tuliongea mwaka uliopita na wazazi wake na tukarudi na kuendelea na maisha, ilifika mahali akaanza kunitusi akisema mimi ni useless, natembea na wanawake wakubwa kimiaka na mimi ni malaya." Aliongeza.

Hata hivyo juhudi zetu za kumpata Hellen hazikufua dafu kwani John alicholilia zaidi ni amani pekee.