PATANISHO: Mke wangu nampenda kama machungwa! - Mburu

Leo katika kitengo cha Patanisho aliyeomba kupatanishwa ni jamaa kwa jina Julius Mburu, 46,  akidai walikosana na mkewe bi Nancy, 42, miezi misita iliyopita.

"NIlikuwa naishi Nairobi naye ushago na tulikosana baada ya watu kunieleza kuwa alikuwa na mipango ya kando. Nilipomuuliza kuhusu madai hayo akaondoka na kwenda kwao."

Mburu aliongeza akidai kuwa kwa miezi sita sasa kila anapojaribu kuzungumza naye mkewe huwa anadinda.

Nataka tupatanishwe kwani nimepeleka mahari tayari na ni wangu!" Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 23 na kifungua mimba wake ana miaka 22 na mkewe ndiye anaishi na wanao.

Bi Nancy alipopigiwa simu alisema kuwa hawezi zungumza sasa hivi kwani yuko kazini. Isitoshe alisema Mburu akawaombe wazazi wake msamaha ila sio yeye.

"Uliwatusi wazazi wangu kwa hivyo sio mimi anaomba msamaha, isitoshe alitusi watoto na kuwakana." Alisema Nancy kabla ya Mburu kumlaumu shetani.

Isitoshe bi Nancy alisema mumewe amekuwa na mazoea kwani hii ni mara ya tatu.

Aki nampenda mke wangu sijui kama nini....labda machungwa! Mburu alijitetea.