PATANISHO: Mke wangu tulikosana baada ya kumpeleka mtoto nyumbani

Ramadhan aliomba apatanishwe na mkewe bi Lucy.

Kisa na maana?

Nilimkosea sana kwani nilichukua mtoto nyumbani. Mtoto alilelewa nyumbani na alipohitimu miaka miwili nikamchukua na kumpeleka nyumbani bila kumweleza na niliporudi tukazushiana.

Ramadhan anasema mtoto alikuwa amelelewa na mamake mzazi na alikuja akaambiwa kuwa mkewe anataka kumchukua na hapo akachukua ile hatua.

"Katika miaka hiyo, mke wangu alikuwa kazi salon nami nilikuwa kazi kwa kampuni fulani na baada ya shida fulani tukafanya maamuzi yale. Tunapozungumza mke wangu yuko mshomoroni nami niko Kisumu." Aliongeza.

Ramadhan alisema akiri makosa na angependa kumuomba msamaha baada ya kuishi kwa ndoa ya miaka kumi.

Kulingana na jamaa huyu, mjombake Lucy anamsubiri aende Mombasa lakini bado hajawezi kwani amepata kibarua hivi majuzi na itabidi ajitahidi kwanza ili apate mda wa kusafiri hadi nyumbani mwa mke wake.

Hata hivyo, juhudi zetu za kumpata bi Lucy hazikufua dafu kwani simu yake ilikuwa imezimwa.

Basi wewe kama mwana jambo swali ni je, wadhani kumuachia mama mtoto husaidia katika malezi na faida zake ni zipi?