PATANISHO: Mume Wangu Alitaka Kukimbia Na Mtoto Hadi Rwanda

Bi, Lorna alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe John.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba baada ya kuchumbiana kwa miaka minne.

Kulingana na mwanadada huyu, walikosana na mumewe wiki moja iliyopita kwani mumewe alitaka kwenda na mtoto waliojaliwa naye, hadi nchini Rwanda.

"Alinipata kwa ndoa nikiwa na mtoto mmoja na pamoja tukajaliwa mtoto mmoja. Sasa alikuwa katika safari akitoka Mombasa akanipigia simu kuwa nitayarishe mtoto anataka kusafiri naye hadi Rwanda. Nami nikamueleza kuwa kama anadai kusafari na mtoto lazima twende pamoja.

Aliniambia pia nijitayarishe twende pamoja lakini nikamueleza kuwa aliniambia mda ukiwa mchache sana na sikuwa na stakabadhi za usafiri. Hapo tukajibizana sana na nikamtusi vibaya sana." Alieleza Lorna huku akiongeza kuwa tangia wakati huo mumewe hajampigia simu na haelewi aliko.

Bwana John alipopigiwa simu alijieleza; "Mimi ni mtu wa masafari ya mbali na nilitaka nisafiri na mtoto wangu na mke wangu lakini nilipopanga safari nikama mke wangu huwa haniamini kwa ajili ya kazi yangu.

Hajanikosea na lolote lile." Alisema John akiongeza kuwa anampenda mkewe na yeye pia anajua vile.

"Kuna siku nilimwambia mume wangu anipeleke kwa nyumba yake Kampala na alinidanganya kuwa hana nyumba na kwa mfuko wake niliona kijikaratasi ambacho alikuwa amelipia GoTV." Aliongeza Lorna huku John akisema kuwa kazi yake iko Kampala kwa hivyo yeye pamoja na madereva wenzake wamekodisha jumba moja mjini humo.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be