PATANISHO: Mume wangu hajawahi peleka hata kuku kwa babangu

Lilian, 21, aliomba apatanishwe na mpenziwe Alex, 39, ambaye wameishi pamoja kwa miaka mitano na wakajaliwa mtoto mmoja.

"Last time alitoka Nairobi ilikuwa ni msimu wa kulima na nikamwambia anisaidie na badala yake akasema kuwa hawezi ambiwa na mwanamke na hapo akanizaba kofi.

Baadaye akaniambia ataniitia mamangu anitoe kwa lile boma kwani hata ndugu zake walitaka kunipiga pia." Alisimulia Lilian.

Hata hivyo juhudi za kumpatanishe Lilian hazikufua dafu.

Hapo tukaamua kuwapatanisha wapenzi wawili, Edward na mkewe bi Rose.

Edward, 35, aliomba apatanishwe na mkewe akidai kuwa mkewe, Rose, 32, alikuwa analalamika kuwa yeye hunywa pombe sana.

"Tumeoana kwa miaka kumi na tuna watoto wawili ambao aliniachia mwanzoni halafu akaja akawachukua, mwaka uliopita." Alisimulia Edward.

Alipopigiwa simu bi Rose, alisema kuwa story yao iliisha na tayari yuko katika ndoa nyingine.

"Sasa mimi nimeshaamua na niko tayari kwa ndoa nyingine nitafanyaje? Wewe si ulikuwa na mwenzako iliendaje mkawachana?" Aliuliza Rose kabla ya Edward kusema kuwa alikuwa na stress.

Alisisitiza kuwa aliamua kuolewa na tayari yuko katika boma lingine. Isitoshe anakiri kuwa Edward huwa hachungi watoto wake na hilo ndilo lilifanya awachukue watoto.

Isitoshe Rose anakiri kuwa Edward hajwahi hata peleka barua nyumbani na kuwa wazazi hata hawajui alikuwa anaishi na nani Nairobi. Alisisitiza kuwa Edward akirudi nyumbani azungumze na wazazi basi atarudi kwa nyumba.

"Mimi mtu hawezi nifanyia madharau hata babangu hajawahi pata hata kuku." Alisema Rose kabla ya kukiri kuwa hajaolewa.