patanisho

PATANISHO: Mume wangu hupea wanawake simu wanitusi

Mercy, mwenye umri wa miaka 26, ndiye aliyeomba kupatanishwa na mumewe bwana Kevo akidai ameshindwa na ndoa yake na anafikiria kujitia kitanzi.

Alipoulizwa mbona kapata mawazo yale, Mercy alisema,

PATANISHO: Nimebaki nikichekwa na Jamaa aliyeninyang’anya mke

“Yaani nimefika mwisho kwani hadi mume wamgu hupea mama mwingine simu anitusi. Mimi nilikuwa nimekubali kuishi ushago huku yeye akiwa Eldoret. Na nikizungumza naye ananiambia kuwa ni mwanadada alichukua simu yake bila yeye kufahamu.
Kulingana na Mercy, cha kushtua ni kuwa yule mama ambaye humtusi anajua siri zao zote ikiwa mipango yake ya ujenzi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba na wamejaliwa watoto wawili ambao wanaishi na mama yao.

Nimevumilia Sana Kwani hata mwaka wa 2015 kuna mama ambaye amezaa naye alinitusi kuwa sijasoma na sipaswi kuwa naye.” Aliongeza Mercy.

PATANISHO: Nilikuwa nalala na kisu kitandani kwa raha zangu

Anasema licha yao kukosana, Kevo alikuwa anashughulikia watoto.

Hata hivyo, hatukuweza kuwapatanisha wawili hawa kwani bwana Kevo hakujibu simu yetu.

 

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments