PATANISHO: Mwanangu hana heshima yeye hunitusi mbele ya mke wake

Boniface alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mamake mzazi ambaye walitengana na babake miaka kumi na mitano iliyopita.
"Mathe waliwachana na fathe na mimi pamoja na ndugu zangu sita tukaenda kwa wazee wa kijiji ili tuweze kumrudisha nyumbani. Kwenda kwa babangu alikataa kurudi nyumbani akisema kuwa walitengana na hayo yakaisha.

Baba yetu naye alituweka ndani na tulipotoka tuling'ang'ana na tukaweza kumrudisha mama nyumbani na tukamjengea nyumba." Alisimulia Bonny.

Alikiri kuwa baada ya mda mama yao alianza kuwabagua watoto wake kulingana na mali anayompelekea akidai kuwa sahii anaskizana na ndugu yake mkuu.

Ndugu yangu alikuwa anapeleka mahari na tukimzindikisha hapo ndio mathe alianza ugomvi nami, alilaani kazi yangu na watoto wangu sasa sielewi shida iko wapi.

Mama Beatrice alipopigiwa simu alisema kuwa mwanawe alimtusi vibaya sana mwaka jana jinsi bwanake alimkataa na kuwa ataleta gari itakayompoteza.

"Huyu hata akipata akienda haja ndogo napitanga kwangu lakini sasa anapitia huko kando ili aende haja ndogo, sasa mimi naye nani ana makosa, Mimi ndio nilimzaa mbona nimsingizie kuwa alinitusi?" Alisema Mama.