patanisho.dope

PATANISHO: Nampenda mke wangu hadi nimemtungia wimbo

Katika awamu ya leo ya Patanisho, Bwana Malit aliomba apatanishwe na mkewe bi Evelyn, ambaye walikosana na akatoroka nyumbani.

“Mke wangu tulikosania maneno ya simu, kupigiwa simu usiku na wanaume na pia tabia ya kukimbia kimbia nyumbani. Najenga reli ya SGR na sasa wakati mke wangu alienda nyumbani aliniambia nimtumie pesa mtoto ni mgonjwa.” Alisema Malit.

PATANISHO: Nilimuuma mke wangu kifuani kwa hasira

Anatumia laini tofauti ya kuomba pesa na kuizima pindi ninapozima. Usiku mmoja nikaenda kwa mamake na kumbe alikuwa amekomboa nyumba. Tukiwa naye akatumia jamaa fulani ujumbe. Yule jamaa alikuwa anamuuliza kwani nani alinionesha anakoishi, naye akamjibu kuwa ni watoto wamenileta.” Aliongeza.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili katika ndoa ya miaka mitano.

Evelyn hakuwa na ubaya na mumewe na amemsamehe ila tu awache matusi na madharau.

PATANISHO: Huyo jamaa akae tu na ujinga wake!

“Sasa hasira zilizidi na ukaanza kunitusi?” Aliuliza Evelyn.

Isitoshe bwana Malik ambaye alikiri kuwa msanii, alimwimbia mpenziwe wimbo alioutunga.

Skiza uhondo wote.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments