PATANISHO: Nashuku mke wangu ana mpango wa kando

James na mkewe bi Agnes akidai walikosana mwezi wa pili mwaka huu huku akisema hajui chenye alimfanyia kulingana na jinsi alivyoondoka.

Nilikuwa naenda matanga nyumbani na wakati nilirudi nikapata jamaa fulani wakizungumza na mke wangu, na siku nilimuuliza nini inaendelea na huyo jamaa akapinga akasema hakuna jambo lolote.

Nikielekea kazini siku moja nikamwambia nikirudi atanielezea hayo maneno vyema lakini niliporudi nyumbani nilipata ameondoka na kwenda kwetu nyumbani.

James anasema kuwa kuna siku alimuendea bi Agnes nyumbani kwao na baada ya siku kadhaa akarudi tena, isitoshe kila mara yeye husema atarudi nyumbani lakini hajawahi rudi.

Mkewe alipopigiwa simu alisema bado hawajasuluhisha maneno yao lakini bado anampenda mumewe kama baba wa watoto wao.