PATANISHO: Nashuku Mtoto Wangu anasumbuliwa na Majini Na Bwanangu Hataki Kutushughulikia

Maureen alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa alipoenda nyumbani kupiga kura mumewe alimueleza asirudi na vitu vyake.

Isitoshe mtoto wao ni mgonjwa na mumewe alipata mke mwingine.

"Nilienda ushago kupiga kura na bado mtoto alikuwa mgonjwa sasa nikamueleza mume wangu kuwa ninamshughulikia mtoto. Kumpigia simu akanielezea nisirudi na dadake alinieleza kuwa nisijishughulishe kwani Abu ameoa tayari." Alieleza Maureen akidai kuwa anashuku kuwa mtoto wao anasumbuliwa na majini.

Maureen aliongeza kuwa kuna siku alimpeleka mtoto hadi kwa jamaa fulani ambaye alimshauri kuwa kuna kitu mama mkwe walimfanyia mtoto.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be