PATANISHO: Nikilipa Deni La Elfu Nane Nataka Lihesabiwe Kama Mahari

patanisho.reloaded
patanisho.reloaded
Kulikuwa na visanga hapo jana katika kitengo cha patanisho baada ya jamaa mmoja aliyefungwa korokoroni kwa kumuoa mtoto wa shule, kudai kuwa walikosana na mama mkwe kwa ajili ya hayo na angetaka apatanishwe.

Baada ya kupewa fursa iliibuka kuwa mama mkwe alikosana na Justin Museti kwani katika pilkapilka ya kumtafuta mwanawe kutoka Kisii hadi Nairobi, alidai arejeshewe fedha alizotumia takriban shilingi elfu nane.

Justin naye hana shida ya kuzilipa zile fedha lakini swala ni je, fedha hizo zitahesabiwa kama mahari?

Kulingana na Justin alipatana na mwanamke wa miaka kumi na sita, barabarani na baada ya kuzungumza kwa mda akampa nambari yake na hapo wakaanza kuishi pamoja baada ya mda mchache.

"Mimi sikuwa na habari kuwa ni mwanafunzi, kumbe ile nambari nilimpa aliwacha kwao nyumbani alipokuja kuishi nami Nairobi. Mamake akachukua nambari ile na kusema kuwa mwanawe ametoweka na angetaka kujua kama ni mimi ndiye niliyekuwa naye, nikamdanganya na hapo nikamuuliza mwanadada kama ni ukweli yeye ni mwanafunzi. Alinieleza kuwa alikuwa mwanafunzi lakini hana hamu ya shule tena, asubuhi moja nikaamka nikapatana na askari ambao walinikamata kwa kuwa na mtoto chini ya umri wa miaka 18." Alisimulia bwana Justin.

"Isitoshe nilifungwa rumande kwa mwaka mmoja huku kesi ikiendelea. Alijifungua mtoto mmoja nikiwa mle ndani na nilipotoka jela baada ya kesi kuisha sasa tunaishi na yule mwanadada kama mke wangu. Tangia kesi hiyo ianze familia yangu na familia ya bibi yangu hazijawahi patana kwana kila mmoja alibeba kisu amdunge mwenzake." Aliidi kusimulia.

"Nilimuambia Justin anirudishie fedha nilizotumia wakti wa kusafiri kutoka Kisii hadi Nairobi kwani ilikuwa ni hasara tupu na hapo akakataa akaja akatorosha msichana sahii wako Nairobi." Alijieleza mama Sylvia huku akimshauri Justin asafiri hadi nyumbani akamuombe msamaha ki rasmi.

Jamaa naye ako tayari kumlipa mama mkwe zile shilingi elfu nane lakini angependa kujua kama zitahesabiwa kama mahari.

Pata uhondo kamili.

&t=18s