PATANISHO: Niliachana na mume wangu kwa maana ana watoto wengi huku nje 'am already booked'

Bwana Davis alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake Lilian ambaye walikuwa wameoana naye kwa muda wa miaka mitano na kubarikiwa na mtoto mmoja na kutengana mwaka wa 2018, Davis alikuwa na haya ya kueleza.
"Nilimsaidia mke wangu kusoma katika chuo kikuu, huku akisomea kazi ya ualimu, baada ya kumaliza alipata kazi karibu na kwao nyumbani alikuwa anamaliza miezi mitano hata bila kurudi nyumbani

Alitoka nyumbani na kuniambia amepata kazi tangu mwaka wa 2017 hajarudi nyumbani, nampigia simu namwambia aje nyumbani lakini  ananiambia napaswa kupatana naye kwa mkahawa

Nikimwambia aje tuishi ananiambia bado anapanga." Alieleza Bwana Davis.

Lilian alikuwa na haya ya kusema,

"Hajawahi ni somesha nilikosana naye kwa maana alikuwa anaenda nje ya ndoa, amezalisha wanawake wengi humu nje kama amebadilisha tabia anitafute tuzungumze

Niliachana naye kitambo ata nimemlea mtoto wangu na hujachangia chochote, amezalisha hata msichana tulikuwa tunalea, cha muhimu aweze kubadilisha tabia nitarudi nyumbani lakini mimi sina haja na yeye kabisa kwa maana amechelewa

Tayari nina mchumba akija nyumbani wacha ajitembeza kwa sasa ."

Bwana Davis, alikana na kusema kuwa hana bwana mwingine, ilhali Lilian alisema kuwa Davis anapaswa kumsaidia mtoto wake kwa maana ni wake.

Kwa Uhondo zaidi tembelea Youtube ya radiojambo.