Patanisho: Nilikosana na mke wangu kutokana na pesa za biashara

NA NICKSON TOSI

Patanisho ni kitengo ambacho huwaleta wawili waliokosana katika jamii ili kuweza kupata suluhisho na iwapo wanaweza kurudiana katika mahusiano.

Hii leo mwanamume kwa jina Joshua alitaka kupatanishwa na mkewe Alice wa ndoa ya miaka zaidi ya 15 baada ya kukosana kuhusiana na pesa za biashara zinazotoka kwa magari yao mawili ya uchukuzi wa uma Nissana na Matatu'' .

Alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema.

Nilikosana na mke wangu Alice kutokana na pesa zilizokuwa zinatokana kwa biashara zetu za magari ya uchukuzi, nilitaka kuuza magari hayo kwa kuwa yalikuwa yamezeeka sana, na pesa hizo nikaweka katika biashara nyingine. Alikataa katakata na kutaka pesa hizo wagawane mia kwa mia, nilipokataa,  alifunganya na kwenda kwao na hata kufunga simu, nimejaribu kadri ya uwezo wangu kujaribu kuzungumza naye lakini hataki kunisikia. Alisema

Alipopigiwa simu Alice alikuwa na haya ya kusema.

Sasa sasa hivi ndio unajua kuomba msamaha, utaamua kurudisha kila kitu ikiwemo magari ndio turudiane? Hiyo pesa uliyouza magari uko nazo kabla nirudi? Ninataka nijue iwapo magari hayo yako. Alice alimuuliza mumewe.

Nikiona magari yote mawili ndio nitarudi na hata ulipouza magari hayo yote mawili sikuona pesa saizi ndio nitakupata nazo? Aliongeza Alice

Alipoulizwa iwapo alitaka wagawane pesa hizo, Alice alikuwa na haya

Aliuza magari hayo na kuweka pesa  kwa biashara ya mahindi ambayo haina hata faida, aliongeza Alice

Niliuza magari hayo yote kwa shilingi milioni 1.3  na kufikia sasa nimepata faida na kufikia shilingi milioni 2. Alisema Jshua.

Aidha Alice alipusilia mbali madai hayo na kusema kuwa ingekuwa bora iwapo mumewe angemtafuta na kuenda kuzungumza na wazazi wake baada ya kuuza magari lakini hakuta kufanya hivyo na kutaka kujivinjari pekee yake.

Mimi sitaki anunue kitu kingine nataka aende anunue magari mawili na turudishe kwa barabara kwa maana magari hayo yalikuwa yanatusaidia sana, hiyo pesa haiko Gidi na Ghost nawaambia ukweli. Alidai Alice

Kwa upande wake Joshua alisema haya.

Hii pesa iko na natamani kuishi na watoto wangu na kama anataka niende kwa  benki nimletee nakala za benki nitafanya hivyo. Alisema Joshua

Huko mimi sirudi, wacha aendelee kufanya biashara vile anataka, na hata watoto wanasoma asiwe na wasiwasi. Alisema Alice.

Msimamo wangu sasa ni yeye arudi nimpatie aende anunue gari lake aweke dereva wake kwa sababu haniamini hata. Aliongeza Joshua.