PATANISHO: Nilimgonga Mke Wangu Na Mtungi Kwa Hasira

Siku ya Jumatano, bwana Patrick aliomba apatanishwe na mkewe, mama Junior ambaye walikosana miezi sita iliyopita. Isitoshe mkewe alitoweka na wanao na hajui waliko.

"Tulikosana na mke wangu mwezi wa kumi. Siku moja nilirudi nyumbani nikapata mke wangu hajafanya kazi ya nyumbani na nilipofika ndipo alipotuma mtoto akachote maji ilhali alishinda nyumbani bila kufanya lolote. Nilikataza mtoto kuchota maji na hapo mke wangu akaanza matusi akikiri kuwa namharibu mtoto na akaanza kunirushia matusi. Hapo nilikasirika na kumgonga kwa ule ule mtungi. Baada ya siku kadhaa nilipata mke wangu hayuko na watoto pia hawako, kumpigia simu akadai kuwa ameondoka na ameelekea nyumbani." Alisema Patrick akiongeza kuwa kila anapompigia simu huongea matusi tu na kukata mawasiliano kati yao.

Kulingana na mkewe, bwanake Patrick ambaye wameoana kwa miaka kumi na minne ndiye aliyemfukuza akimuarifu atoke na aende zake.

"Kama unataka nirudi kwako nilikueleza uje nyumbani uongee na wazazi. Muelewane kuhusu mahari halafu ndio nitakuja."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be