PATANISHO: Nilimpiga Mke Wangu Kwani Alikua Anafuatana Na Afisa Wa Polisi

Paul Collins alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Miriam akidai kuwa alimpiga baada ya kugundua kuwa mkewe aalikuwa anafuatana na askari wa polisi ambaye alitaka amsaidie kuingia katika kikosi cha polisi.

"Kuna jamaa fulani ambaye anataka kumsaidia kuingia katika idara ya polisi. Bado nafuatilia hayo maneno kwani jamaa hawezi kuja kwangu na aanze kumpeleka anakotaka. Sasa nikamuuliza mke wangu kuwa ningependa kukutana na yule jamaa na hapo ndio ugomvi ulianza.

Huku nikimuulize mke wangu alidai kuwa yule jamaa alimuahidi kuwa atamsaidia kuingia kwa idara ya polisi. Nikimuuliza mke wangu ananuna na hapo nikamzaba kofi." Alieleza Collins akidai yule jamaa ameachana na mke wake na anashuku kuwa anataka uhusiano na mkewe.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili.

&feature=youtu.be