pata.pata

PATANISHO: Nilimtusi mke wangu kuwa tunda lake sio tamu

Joshua kutoka maeneo ya Kilifi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bibi yake bi Anette akiomba ndoa yake iokolewe kwani yazama.

“Mimi na yeye tumeoana kwa miaka mitatu na alipofika nyumbani sijui ni kama hakupendelea maeneo yale kwani kitambo tulikuwa twaishi Malindi.

Tuliporudi Kilifi ni kama hakufurahia na tulichokosana zaidi ni kuwa alikuwa anateteshana na mamangu na mimi kidogo nikaegemea upande wa mama.” Alieleza Joshua.

Tazama mitaa Sonko wa Redio Jambo atafungia zoezi la kugawa hela nchini

Licha ya yale yote mkewe bado yuko lakini anasema kuna wakati alimtusi na kumwambia tunda lake la ndoa sio tamu. Hata baada ya kuzungumza bado anahisi mkewe hayuko sawa.

“Halafu unajua amepata kazi maeneo ya Tana River na nahofia nitawachwa, huo ndio wasiwasi wangu hata nakonda.” Aliongeza.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Isitoshe Joshua alisema kuwa mkewe itabidi adjust time table ya Mombasa raha kwani hatosheki lakini mkewe anasema hana shida na tendo la ndoa.

Unachotakiwa kufanya ili ushinde elfu 5 na elfu 1 kutoka Redio Jambo

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments