PATANISHO: Nilishiriki mapenzi na mke wa ndugu yangu - Dishon

Dishon Omusini, 26, ndiye aliyetuma ujumbe wa patanisho akiomba wapatane na nduguye bwana Kennedy, 28, akidai kuwa alimkosea sana kwa kufanya mapenzi na mkewe.
"Sijui ni nini ilikuja kwa akili yangu sijui kama ni shetani juu haikuwa kupenda kwangu. Nilikuwa nimewachwa kwa nyumba na ndugu yangu single room. Kuna siku alirejea saa  nne usiku ndio akanifumania nikifanya hayo maneno." Alisimulia Dishon akisema mke wa ndugu yake alikuwa anamtamani.

Aliongeza,

Aliniambia wacha tufanye mara moja kwani hatajua, baada ya ndugu yangu kunipata akachukua virago vyake na kuondoka kabla yangu kuondoka."

Tukio hili lilitokea mwaka uliopita mwezi wa kumi baada ya kuishi na nduguye kwa miezi mitano.

"Mambo yake staki kuskia nilimwambia kama anataka tuzungumze twende kwa wazazi Kwanza ili tuskizane." Alisema bwana Kennedy alipopigiwa simu.

Aliongeza akimshauri na kumpa masharti nduguye,

Enda kwa wazee uwaambie jambo ulifanya sahii Sina mke kwa ajili yako, ulisambaratisha ndoa yangu.

Alisema hadi sahii bado anakwazika moyoni.

Dishon kwa upande wake ana uwoga atapigwa nyumbani.