PATANISHO: Nime register line tano na bado mpenzi haniongeleshi

Dennis akiomba apatanishwe na mpenziwe bi Cecil akisema alimkosea na ana stress kwa hilo, isitoshe alipata ajali wiki mbili zilizopita kwa ajili ya hilo.

"Kuna vile tu nilimkosea mpenzi wangu na akaamua kuniwacha. Ilikuwa last year nilikuwa nimetoka Nakuru then nikaenda kwa cousin yangu Bungoma ambaye ana clinic.

Mwezi wa nne akaenda kufanyiwa scanning akapatikana na ovarian cyst na hapo alipata stress na hakutaka nimuongeleshe." Alisimulia bwana Dennis.

Kulingana na Dennis wawili hao walifungua biashara ya Chemist baada ya Cecil kumpa elfu sabini na sasa ana shangaa mbona mpenziwe hataki kuzungumza naye na kwa nini amemuachia ile biashara.

Hata hivyo juhudo zetu za kumpata cecil hazikufua dafu kwani cecil hakutaka kuzungumza nasi wala bwana Dennis.

Gidi na Ghost walimshauri kutubu dhambi zake na kuomba uelekezi kutoka kwa mungu ili ajue jinsi ya kuendesha biashara ya Chemist.