PATANISHO: Nimemuekea mke wangu biashara lakini hatulii ana vituko kila kuchao

Jennifer alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake Justus Musembi waliokosana Juni waka huu baada ya mume wake kuja nyumbani akiwa amelewa chakari.
"Baada ya kutoka katika ndoa yangu nataka kurudi licha ya ulevi wake kwa maana tunapendana sana, tumekuwa tukizungumza baada ya kutoka wakati mwingine nikimpigia simu anaanza matusi

Alikuwa na bibi wa kwanza na kisha akaenda, nilikuwa napigiwa simu naambiwa kuwa amepata mke mwingine licha ya kutengana mwezi jana

Nilikuwa nikiongea na yeye naona ni kama amerudiana na bibi wake wa kwanza, lakini nataka turudiane kwa maana mimi nampenda sana si kwa sababu nilisikia ameoa." Alieleza Jennifer.

Mumewe alipopigiwa simu alimshauri mkewe akomeshe vituko, huku Jennifer akisema kuwa pia naye anapaswa kukomesha vituko vyake.

"Unapaswa kupunguza na wala si kupunguza ni kukomesha vituko ambavyo uko navyo, kama nilikutisha ungeenda kuripoti kwenye kituo cha polisi

Nimemuekea kazi lakini hatulii, amenipa mawazo mpaka najipata nimeenda kulewa, kwa kweli mimi nitapunguza ulevi."

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao ya kijamii ya youtube.