PATANISHO: Nitamrudia Mume wangu mwaka wa 2022

Mathew wafula nalituma ujumbe akiomba apataniswe na mkewe bi Josephine.
Nilikuwa nakunywa kabla tuoabe lakini nilikuwa na kunywa Sana na tukakosana na mke wangu. Sikumoja nikienda kazini kurudi nyumbani sikumpata. Ilikuwa tarehe 11 mwezi wa February.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa tangia mwaka wa 2014 na aliondoka na watoto wawili.

Alikodisha nyumba hapo karibu na mimi na sisi huonana kila siku lakini hafujawahi rudiana. Hata hivyo Mathew amekiri kuwa tangia mkewe aondoke alipunguza uraibu wa pombe.

Josephine alipopigiwa simu alikiri kuwa alikosewa sana na hawezi rudiana naye. Isitoshe mumewe amejawa matusi na hashughulikii watoto wala mambo ya nyumbani.

"Mimi hufanya kazi ya salon na kufulia watu na sometimes nikirudi nyumbani yeye husema kuwa nimetoka umalaya. Na hayo yamekuwa yakifanyika tangia 2014"Alisema Josephine.

Akizungumza naye, Josephine alimwambia mumewe kuwa ile siku atabadilika kitabia ndio atarudiana naye huku akidai atarudi mwaka wa 2022.

"2022 naona ni ngumu kiasi kwangu"