PATANISHO: Shida zetu zilianza baada ya mume wangu kuanza kuuza Muguka

Julia, 33, kutoka eneo la Lamu pwani aliomba apatanishwe na mumewe bwana Peter mwenye umri wa miaka 50.

"Tulikosana mwaka Jana mwezi wa kumi. Hapo nyuma alikuwa anafanya Kazi ya mjengo na kuwacha na alipoanza kuuza muguka hapo ndio shida ilitokea." Alisema.

Aliongeza,

Nilijaribu kuambia wazazi wake wamkanye na walisema Niwache afanye ila tabia zake zilibadilika kama kunijibu na Isitoshe alikuwa na mpango wa Kando, jambo alilokiri."

Siku moja nikienda kazini kumuomba pesa za chakula alinipiga vibaya na kuning'oa meno ya hapa mbele.

Julia anasema angependa mumewe atumie njia ya kwenda nyumbani kwao ili warudiane.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

" Lazima niketi Chini na wazazi wakikubali Kisha tutaenda kwa kina Julia.

Mke wangu alileta vituko na hilo likafanya achukiwe kwetu nyumbani. " Alisema bwana Peter.