Gidi

Patanisho sio ya waluhya pekee! Gidi na Ghost wakosoa wakenya (AUDIO)

Kwa miaka kadhaa kumekuwa na dhana kutoka kwa wakenya, haswa wasioskiza kituo cha Radio Jambo na sanasana, kitengo cha Patanisho.

Dhana hii ni kuwa juhudi za Gidi na Ghost za kuwapatanisha wawili waliokosana huwalenga tu wana ndoa kutoka jamii ya Luhya. Wengi husema kuwa ni nadra sana uskie kuwa wanaotaka kupatanishwe na watu kutoka jamii zingine.

PATANISHO: Mke wangu alimwaga nyama na akakula fare!

Walichosahau ni kuwa; Patanisho pia huwaleta pamoja hata wafanyi kazi na waajiri wao kutoka lugha tofauti, kwani sio kila mara wana ndoa.

Baaada ya kuchosha na wanaotoa matamshi hayo katika mitandao ya kijamii, Gidi aliamua kuzungumzia hayo kabla ya kuwapatanisha bwana Kimani na bi Purity ambao ni wa jamii ya Kikuyu.

Gidi alisema;

“Unaona sasa hivi, tunapatanisha watu wengine halafu wengine bado wanaingia kwa mitandao kusema eti patanisho ni ya waluhya.”

Ghost naye alimuunga mkono akisema,

“Hata jana nilikuwa na mtu ananiambia hivyo nikamwambia my friend Patanisho is for the whole country. Kila mtu ambaye ana matatizo, kwa sababu ndoa sio ya waluhya ndoa ni ya watu wote na watu wanakosana kila mara, kwa hivyo ni kitu cha kawaida jamani.”

PATANISHO: Tulikosana na boss wangu kwa ajili ya kifaa cha sh200

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments