PATANISHO: Sitaki mwanaume kwangu tena, sitaki kuitwa bibi ya mtu tena, nikae hivyo asema Bi Ida

Sitaki mwanaume kwangu tena, sitaki kuitwa bibi ya mtu tena, nikae hivyo.

Haya ndio maneno makali kati ya wapendwa wawili katika kitengo cha patanisho.  Gidi and Ghost walibaki midomo wazi baada ya kuskiza mabishano ya Simon na Ida.

Ida alitoroka mwaka 2016, na Simon alisumulia kilicho tokea.

'Ni kitambo, na bado tunaongea, na anasemanga harudi.'

Mbona anafuatana na yeye?

'Nafuatane na yeye kwasababu alienda na mtoto mmoja wetu, akaniwacha na mwingine. Tuko na watoto wawili, na nataka turudiane aangalie boma yetu. Tulikosanea maneno ya watu. Na deal na transport ya wamama, nawapelekea mizigo sokoni na pick up. Na kwa hiyo harakati akaambiwa maneno, akahesbaiwa ati niko na wamama kumi. Na mimi nikakubali wote ni wangu juu nilikuwa nawabebea mizigo ata tulikuwa tunaenda safari usiku nao, sasa ukienda huko unaskia manene. Hiyo yote nilivumulia. 

Baadaye siku moja nikaenda sokoni kurudi nyumbani nikapata ametoka na mizigo. Akaenda pia na mtoto mmoja. 

Wawili hawa wamekaa miaka fifteen kwa ndoa,

Alipopigiwa simu, Bi Ida alisimulia ile kitu ilitendeka.

aie turudiane? Muulize alikuwa na bibi wangapi nikiwa kwake na nimenyamaza tuu? Alafu muulize..wakati aliniioa hakuwa na chochote? Na tukafanikiwa tukanunua plot mbili, tulikuwa na gari nne tulikuwa tumenunua acre mbili na tulikuwa na pick up ingine, muulize hizo viu zote alipeleka wapi? Na nikimuuliza ananiuliza kwani kuna title yako iko hapo? 

Kwa hivyo sioni haja niake nikiteseka tangu anioe nimekuwa kwake 16 years na mpaka mara kwa mwisho alinifukuza na akaniambia yule mtoto wetu wa kiume si wake, nimpeleke kwa bab yake. nikaona hakuna haja nikae nikisumbuka.

Bwana Simon alijitetea aje?

umesikia hiyo yote eeh mimi nimeuza lakini..skiza mimi huwa nafanya business, unaelewa, akiuliza pesa nimepeleka wapi..ile kitu ilitendeka Boma yangu niliona ni kama oppposition iliangia muulize si akon na plot, si alinunua yake? mimi sikawahi jua iko wapi, Skiza Gidi, huo mke nilikuwa nimemea ruhusa hata sijui mpaka ngombe napata ameuza na sijawahi muuliza 

Kwa hivyo Simon anasema akon na uhuru wa kuuza mali yake bila ya kuulizwa maswali?

Apana sijasema hivyo, nasema hivi, ile kitu inaweza kuwa ni mukae mujadiliane. 

Mbali na haya Simon aliomba msamaha kwa bibi yake, lakini Ida akakataa kuvumilia, akisema amejipanga.