PATANISHO: Solomon na Joyce washindwa kupatanishwa baada ya kukata simu

Siku ya leo Monday October 17th, Solomon Ongaro wa miaka 26, alitaka kupatanishwa na mkewe wa miaka 21, ambaye alimuuacha, na kuenda kuishi na pastor mmoja kijijini.

Aliweza kuarifu Gidi and Ghost kwamba mke wake alitoroka boma yake na amekatalia kwa nyumba ya pastor, baada ya kuwachana na yeye.

Bwana Solomon aliuliza usaidizi wa Gidi kumpatanisha na bibi kwasababu amejaribu kumwongelesha, lakini amekatalia kwa pastor, huku akisema anatamani arudi kwasababu watoto wao baado wako wachanga.

Solomon ameshindwa ni vipi pastor amemfanyia bibi yake, kwasababu huyu jamaa pia ana bibi wake.

Bwana Solomon alisema bibi yake hashugulikii watoto wake, na 'hata nikimwongelesha, anasema hatarudi kwangu, ameamua kunitoroka'.

Gidi alimpigia mke wa huyu jamaa kwa kupitia simu.

Joyce aliweza kuchukuwa simu, lakini alipo julishwa ni Radio jambo alikata simu.

Gidi akapigia Solomon kumjulisha kwamba alikata simu walipoanza kuongea.

Lakini Solomon alimuomba Gidi apige simu tena, aone kama ataweza kuongea tena.

Kwa mara ya pili, Gidi alipiga simu tena, amhoji tena, ambembeleze wapatinshwe.

Na kwa kweli ya mungu ni mengi!!

Alikataa kuzungumza lakini mkewe Solomon akamwambia mumewe kwamba 'sitaki ujinga'.

Akaendelea kusema 'yangu na yako iliisha', na asiwahi kunisumbua, na asipige simu tena'.

'Nilimwambia anipatie watoto akakataa, na asinipigie watoto'.

Bibi yake hapo akakata simu. Lakini Solomon hakukufa moyo. Alishauri Gidi apige mara ya tatu.

Gidi pia alipigia Pastor, na mchungaji na akajulishwa kwamba Solomon anauliza kama pastor anaweza kuwapatanisha.

Mchungaji aliarifu Gidi kwamba huyo mama amekataa kurudiana na bwanake. Pastor alisema kwamba mkewe Solomon anaishi na yeye kwasababu hakuwa na pahala pa kuishi kwasababu wazazi wake walikufa'.

Alisema,' she had nowhere to go, and I volunteered a place for her to stay. Mimi kama mchungaji siwezi na sina uwezo wa kulazimisha bibi arudi kwake kama hataki'.

Skiza kanda ifuatayo;