PATANISHO: Tafadhali Toa Huto Tushetani Kichwani Mwako

Beatrice alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bwanake Chris ambaye walikosana siku ya Jumapili kwa yale alitaja kama kutoelewana kwa nyumba.

"Nilielekea kanisani huku nikumuacha mume wangu na mtoto wangu na baadaye nikaelekea shughuli yangu. Niliporudi nyumbani nikapata kama ameeleza dada yangu kuwa niliondoka bila kumuachia mtoto maziwa na hapo nikakasirika huku nikimueleza jambo kama hilo huenda likaharibu ndoa, hapo akanigombanisha na akaanza kuninyonga.

Nikamsukuma kwani nilikuwa naumia na tangia siku hiyo hatuzungumzi kwa nyumba ingawa tunaishi pamoja." Alijieleza Beatrice.

Alipopigiwa simu bwana Chris alieleza kuwa akitoka nyumbani asubuhi alikuwa amesuluhisha kila kitu kuhusiana na ugomvi wao na kuwa alishtuka kwamba mkewe alipeleka ujumbe redioni.

"Shida ilikuwa ni ugomvi kati yake na dadake na hapo nikawaeleza kuwa sitaki hayo maneno hakukuwa na mambo mengi. Sasa hata nimestaajabu kuwa amewaeleza kuwa tuna shida." Alisema Chris.

Hata nilikuwa nimedhani nimeshinda pesa katika Radio Jambo cash call, nimeshtuka bana." Aliongeza huku akimuambia atoe kashetani kadogo kaliko kichwani chake.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be