PATANISHO: Tangia Novemba mwaka jana sijui mke wangu aliko

Vincent alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Esther ambaye walikosana mwezi Novemba mwaka uliopita.

Ilikuwa Novemba mwaka uliopita na sijui aliko kwani nikimpigia simu ni kelele tu na sana sana anani black list hachukui simu. Isitoshe aliondoka na watoto wetu wawili.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane.

"Nilikuwa na rafiki kabla tuanze maisha naye na yule msichana tukapata mtoto naye, alipo olewa alitaka kuniletea mtoto na hapo mabishano yakaanza kati yangu na mke wangu." Alielezea Vincent.

Alidai kuwa amejaribu kwenda kwa wazazi lakini mkewe hapatikani ili wakasuluhishe maneno kati yao.

Hata hivyo juhudi zetu za kumtafuta bi Esther hazikufua dafu.