PATANISHO:Mke wangu alienda kwao nilipolala nje usiku mmoja

Bwana Kennedy Kipyegon alituma ujumbe apatanishwe na mke wake Nelly waliokasana wiki tatu zilizopita hii ni baada ya bwana huyo kulala nje usiku mmoja.
"Mimi na fanya kazi ya kusafirisha nyanya kutoka shambani wakati ambao ni lala nje hatukuwa tumepata nyanya za kutosha za kusafirisha

nilipigoa mke wangu simu lakini simu yake ilikuwa mteja, nilituma jirani ili amwambie kuwa sitarudi nyumbani lakini mtumwa hakufikisha habari yenyewe

niliporudi kutoka kazini nilipata amekusanya virago na kuenda,nilipoenda kwao baba mkwe alileta shida nyingi sana." Alieleza Kennedy.

Naam lakini kuna kitu Kennedy alificha ambacho kilifichuliwa na mke wake? huu hapa usemi wa mkewe.

"NIlienda kwetu kwa maana Kipyegon ana mpango wa kando ambaye anafahamika kama Brenda, nilikuwa naona mpaka kwa jumbe za simu akimwambia kuwa anampenda

lakini akiachana na huyo Brenda naweza kurudi na tuendelee na ndoa yetu."

Bwana huyo alikubali makosa yake ya kuwa anampango wa kando na kuapa kuwa hatakuwa naye tena.