Patanisho:Mke wangu aliniacha baada ya kuhudhuria sherehe

Bwana Wambua alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake ambaye walikosana naye baada ya kuenda sherehe kwa nyanya yake, aliporudi alimpata mkewe ameondoka.
"Niliondoka na kuenda kwa nyanya yangu kwa sherehe, nilienda mpaka kwao lakini hakuwa amefika kwao, nilijulisha naenda kwenye sherehe hiyo lakin hakukubaliana nami

Hajaniambia sababu yake ya kuondoka,kwa maana hatukuwa tumekosana awali, sikuwa na mipango ya kando sijawahi mkosea." Wambua Alieleza.

Wambua alidai kuwa alizungumza na mkewe kisha akamtumia nauli bali hakurudi, baada ya hayo alimpigia simu na kumwambia kuwa ata mwambia nini haswa kilitendeka ili aweze kuondoka nyumbani kwake.

"NImejaribu kuzungumza na baba yake na akaniambia kuwa atarekebisha mambo lakini sijaona chochote, kwa kweli naumia sana." Wambua Aliongea.

Je ni ushauri upi unaweza kumpa bwana huyo?