PATANISHO:Mume wangu amekuwa akinipiga akisikia vita kunihusu

Bi Mary alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe ambaye walikosana Agosti mwaka huu hii ni baada ya kusikiza vita kutoka kwa familia yake na kuanza kumchapa.

"Tumebarikiwa na mtoto mmoja nilikosana na mume wangu baada ya kila mara kusikiza vitina na kuanza kunichapa, huwa analewa nataka abadilishe hiyo tabia ili uweze kumlea mtoto wetu

Akiwa kazini anapewa vitina na jamaa zake kuwa nimeonekana na mwanamume mwingine." Mary Alisema.

Bwana otindo naye alikuwa na haya ya kusema;

"Huyu mwanamke alienda sherehe iliokuwa nyumbani kwao na kukwamia kwao nilipompigia simu na kumuuliza kwanini hajarudi aliniambia kuwa hatarudi

nilinyamaza tu, mimi nilimwambia nitabadilisha tabia zangu na arudi nyumbani kwa maana bado mimi nampenda kama peremende." Alizungumza.