PATANISHO:Mume wangu amekuwa akitoka kazini, anabadilisha, anaondoka na kurudi asubuhi akiwa amelewa chakari

Mama Ivy, 27, alituma ujumbe ili apatanishwe na mumewe 33, ambaye wamekuwa wakikosana naye tangu Januari mwaka huu, ujumbe wake ulisema kuwa mumewe amekuwa akitoka kazini baada ya kufika nyumbani anabadilisha nguo na kwenda anarudi kesho yake akiwa amelewa chakari cha mno mumewe hakuwa anamuachia pesa za chakula.

Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja.

"Nilikuwa mashambani mume wangu alinipigia simu na kuniambia niende kuishi naye Mombasa, alianza hiyo tabia tangu nianze kuishi na yeye namuuliza nini mbaya hanijibu

Akitoka kazi anapata nimemtayarishia kila kitu, mpaka nampapasa lakini nashindwa shida ni gani, huwa ananiambia anaenda kwa dakika thelathini lakini hizo dakika zinakuwa usiku mzima

Nimemwambia anijengee nyumba bara lakini haniskizi." Mama Ivy Alieleza.

Baba Ivy alipopigiwa simu alikuwa na hayo ya kusema,

"Mbona hukuniuliza swali hilo nikiwa nyumbani, kwa sasa mahali niko siwezi zungumza nikirudi nyumbani tutazungumza kuhusu jambo hilo."

Je, unaweza kuwapa ushauri upi kabla ya mkewe kuondoka na kurudi kwao?