Patrick Akubali Kumsamehe Mwanawe Aliyemtusi Kupitia Facebook

patrick
patrick

Katika makala ya patanisho, kisa kimoja kilizuka wakati Evans alipo omba apatanishwe na babake bwaba, Patrick ambaye walikuwa wamekosana kwa mda wa mwezi mmoja. Kisa na maana; Evans alimkasirikia babake na kumtusi kupitia ukurusa wa Facebook.

Kulingana na Evans, haya yote yalisababishwa na mzee "Kuingilia ndoa yake" jambo ambalo halikumfurahisha.

Alishangaza wengi alipokiri kuwa aliwahi kunywa sumu ili ajitoe uhai na babake hakumsaidia licha ya shida aliokuwa nazo za kindoa na pia za kimwili.

Isitoshe, babake kwa upendo wote alimsamehe yote na kumkubali tena kama mwanawe lakini lazima arudi nyumbani ili wazungumze wasuluhishe yote.

Skiza kanda ifuatayo.