Mgomo huo wa madaktari nchini Zimbwabwe umesababisha vifo vya watu kadhaa na umekuwa mojawapo ya migomo iliyodumu muda mrefu sana nchini humo. Bwenyenye huyo amewapa madaktari ofa hiyo nzuri na wemekubali kurejea kazini. Madaktari wengi wanaoshiriki mgomo huo hulipwa chini ya dola 100 kwa mwezi . Ufadhili wa bilionea huyo utadumu kwa miezi sita lakini haijafahamika kitafuata kipi baada ya muda huo.
Madaktari wanaogoma wamekuwa wakitaka kuongezwa mishahara ili kuweza kukimu gharama iliyopanda ya maisha nchini humo kwa ajili ya hali mbaya ya uchumi wa Zimbabwe .
Strive Masiyiwa ni nani?
Mzaliwa huyu wa Zimbabwe alizaliwa mwaka wa 1961 na kwa sasa anaishi mjini London. Ni mmiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Econet Wireless. Mali yake inakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za kimarekani bilioni 1.1(mwaka wa 2020).