PICHA: Baada ya kutesa Mombasa Massawe asafiri hadi Dubai

Massawe Turkey
Massawe Turkey
Takriban miezi miwili iliyopita, mtangazaji hodari Massawe Japanni alifunga safari na kuelekea hadi Mombasa kwa kipindi cha wikendi nzima kwa mujibu wa kusherehekea birthday yake.

Mtangazaji huyu mrembo kupindukia wa kipindi cha Bustani la Massawe, pamoja na marafiki zake wa ngazi ya juu walijibamba kupindukia ndani na pia nje ya bahari, huku 'akitesa' kwenye mtandao wa Instagram.

Akiwa huko, Massawe alipata fursa ya kukata keki pamoja na wapendwa wake huku akiendelea kuburudika katika likizo yake ndogo.

Miezi miwili badae Massawe ameamua kuchua breki kidogo na kusafiri hadi Dubai ili kuhepa kelele za Nairobi na pia ili kupata fursa ya kupumzika na kupunga unyunyu kiasi.

https://www.instagram.com/p/B2slzqtADBt/

Kupitia Instagram, mtangazaji huyu mama wa watotot watatu, alichapisha picha kadhaa akiwa safarani na pindi tu mashabiki walitaka kujua aliko, aliwajulisha kuwa alikuwa safarini akielekea Dubai.

Isitoshe, alimwambia shabiki mmoja kuwa wiki hii yote hatokuwa hewani kwa kipindi chake ambacho huja kuanzia mida ya saa nne asubuhi, kwani bado hatokuwa amerudi.

Bado haijulikani Massawe atakuwa Dubai kwa mda upi wala hamna ajue aliyesafiri naye kwani sasa hivi hawezi safiri na wanawe hadi watakapounga shule.

Hata hivyo, hii leo alichapisha picha yake akiwa Uturuki na hatuna uhakika kama atakuwa anatalii mataifa tofauti katika likizo yake.

https://www.instagram.com/p/B2s0MUoAHmE/

Mapema mwaka huu, mtangazaji huyu nguli pamoja na wanawe walisafiri hadi Italia kwa siku kadhaa kwa likizo ya kukata na shoka. Wakiwahumo waliweza kutembelea majumba ya makumbusho, miji mikuu kama Verona na Venice na maeneo mengine mengi.

Huku akijibamba, mtangazaji Eudias Kigai ndite atakayeshikilia usukani.