ken.okoth.na.Angelina.Ajwang.

PICHA: Mamake Ken Okoth apiga kura katika uchaguzi mdogo Kibra

Uchaguzi mdogo wa Kibra unaendelea vyema huku kiongozi wa ODM Raila Odinga akipiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera.

 

Mwaniaji wa ODM Imran Okoth ambaye ni nduguye marehemu Ken Okoth, aliwasili kupiga kura akiandamana na mamake mzazi, bi Angelina Ajwang’.

Rekodi ya asilimia 100 ya Arsenal yafika kikomo katika ligi ya Europa

Licha ya visa vichache vya majina ya watu kukosekana kwenye sajili, hakuna kisa kingine kilichoripotiwa kufikia sasa.

Hayo yakijiri, iwapo wewe ni mpiga kura wa Kibra na kituo chako cha kupigia kura ni shule ya msingi au ya upili ya Olympic, basi unashauriwa kuwa kituo hicho kimehamishwa hadi shule ya msingi ya Ayany.

PATANISHO: Nakupenda kuliko avocados! Tusipatie shetani nafasi

Kituo cha Raila Education Centre kimehamishwa hadi shule ya msingi ya Kibera huku kituo cha Upper Hill kikihamishwa hadi kwa hema nje yake.

Tazama picha za Imran Okoth pamoja na mamake mzazi Angelina Ajwang.

ken.okoth.na.Angelina.Ajwang. Angelina.Ajwang Angelina.Ajwang.1

Video ya siku: Mesut Ozil awatuza mashabiki wa Arsenal kutoka Kenya

Photo Credits: Douglas Okiddy

Read More:

Comments

comments