PICHA: McDonald Mariga akabidhiwa cheti cha Jubilee

mariga
mariga
Ni furaha kuu kwa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Harambee Stars, McDonald Mariga baada ya chama cha Jubilee kumkabidhi cheti cha uteuzi.

Mariga pamoja na maafisa wa Jubilee wanatarajiwa kupeleka vyeti vyao katika afisi ya IEBC leo mida ya saa kumi jioni wakingoja kupewa kibali cha kuwania kiti cha ubunge cha Kibera, November 7.

Akimpokeza cheti Mariga, katibu mkuu wa chama hicho, Raphael Tuju aliwarai wagombeaji kuwa na mda wa kampeini na pia uchaguzu wenye amani.

"Tunafaa kukumbuka kuwa kutakuwa na mshindi na anayeshindwa lakini sote tutabakia kuwa wakenya." Alisema.

Mariga alishukuru chama chake kwa kumuamini na kuwahakikishia kuwa ana uwezo wa kupambana na wenzake.

"Kazi ianze sasa..imebaki kwenda kwa mafans." Mariga alisema.

Mariga aliandamana na wabunge kama; Didmas Barasa (Kimilili), Caleb Kositany (Soy), Nixon Korir (Lang'ata) na Gladys Shollei (Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Uasin Gishu).