PICHA: Mwanawe Arocho asafiri hadi China kwa mafunzo ya soka

Mtangazaji, Fred Arocho na mkewe, Sophie ni miongoni mwa wazazi wenye furaha chungu nzima baada ya mwanao, Jayde Arocho, kuchaguliwa kushiriki katika mafunzo ya soka Uchina.

Jayde alichaguliwa miongoni mwa mamia ya watoto nchini kupitia shule ya soka inayo ongozwa na aliyekuwa nahodha wa Harambee Stars, Musa Otieno.

Wachezaji hao wachanga ambao watakua Uchina kwa siku kumi, watapata fursa ya kupata mafunzo ya soka kutoka kwa wataalumu mbali mbali, ili kuboresha taaluma hiyo mapema.

Jayde, 8, ambaye ni strika machachari, aliibuka mshambulizi bora mwaka uliopita katika kituo cha Moi katika kitengo cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 9.

Shirika hilo la Musa Otieno lilichagua takriban wachezaji 22 kutoka shule kadha wa kadha za soka mjini Nairobi, huku Mlolongo na Mbotela zikiwa miongoni mwa mitaa iliyofaidika.

Kama jinsi alivyo imarika katika safu ya ushambulizi, aliyekuwa kiungo wa Atletico Madrid, Antoine Grizman, ndiye mchezaji anaye enziwa sana na mwanawe Arocho.

Ni dhahiri kuwa Jayde anafuata nyayo za babake, Fred Arocho ambaye alizichezea klabu kadhaa humu nchi katika ligi kuu ya Kenya, ikiwemo timu ya KCB.

Arocho aliyejawa na furaha baada ya kupokea ile habari alisema kuwa anajivunia kuwa babake Jayde na ana matumaini kuwa nyota yake itazidi kung'aa hadi siku za usoni.

"Nina furaha sana kwa mwanangu yuko China kupata mafunzo ya soka kwani ukilinganisha nami, sikupata fursa kama hiyo nikiwa mchanga, kwa hilo najivunia sana.

Mwanangu anapenda soka sana na nina imani kuwa atafikia malengo yake kupitia talanta yake." Alisema mtangazaji huyo wa Weekend warm up.