(+Picha) Taswira ya picha za kinyonge ,Peter Mugure yupo jela ya Nanyuki

Screenshot_from_2019_12_06_11_47_03__1575622045_41471
Screenshot_from_2019_12_06_11_47_03__1575622045_41471
Picha za aliyekuwa afisa wa jeshi Peter Mugure zimesambaa na kuteka hisia za wengi katika mtandao.

Mugure ni mshukiwa mkuu katika kifo cha mkewe na wanawe.

Kisa cha mauti ya kinyama ya mkewe na watotoa kiliwashangaza wengi kwa mara ya kwanza kilipotangazwa katika vymbo vya habari.

Jacob Mureithi na ambaye ni afisa mkuu wa polisi eneo la Nanyuki alisema kuwa wachumba hao hawakuwa na mahusiano mazuri.

Maafisa wa upelelezi baadaye walipata simu ya mama watoto ndani ya gari ya kampuni ya 4NTE.

Picha hizi za Mugure zinaonyesha akiwa hoi 'nyumbani kwake' jela la Nanyuki.

Taarifa zipo kuwa huenda akashtakiwa Jumatatu wiki ijayo pamoja na washukiwa wengine wawili.

Polisi wanachunguza kwa umakini ili kubaini sababu kuu za kifo cha Joyce Syombua, Shanice Maua na Prince Michael.