Picha ya siku: Mtindo mpya wa mavazi yake mama Diamond wafurahisha wengi

Katika mtandao wa Instagram, mamake Diamond Platnumz, Sanura Kasimu, almaarufu, @Mama_dangote , amewafurahisha wengi baada ya kuonesha mtindo wake mpya wa mavazi.

Kawaida yake, mama Dangote huvalia, Dera au mavazi ya vitenge yanayopendwa sana barani Afrika.

Hata hivyo, wakti ambapo hana shughuli nyingi na anabarizi tu nyumbani kwake, mama huyu huvalia kaptura au suruali ndefu. Lakini amewashtua wengi na kupendeza mashabiki wake baada ya kuchapisha picha yake akiwa na mavazi ambayo huvaliwa sana na kizazi kipya.

Sanura anaonekana akiwa na shati nyeusi, suruali ijulikanayo kama 'cargo pants' na viatu aina ya Airforce vya rangi ya njano.

Tazama picha ifuatayo.

https://www.instagram.com/p/B8apxnQh0rK/

https://www.instagram.com/p/B8TPUJ3B4vx/