Picha za siku: Bingwa Eliud Kipchoge awasili nchini

Bingwa wa Olimpiki na anayeshikilia rekodi ya mbio za Marathon duniani, Eliud Kipchoge amewasili nyumbani.

Kipchoge amerejea takriban siku nne baada ya kuandikisha historia kama binadamu wa kwanza kukimbia na kumaliza mbio za nyika chini ya masaa mawili, katika mbio za Eneo challenge.

Hii leo, shirika la ndege la Kenya Airways lilichapisha ujumbe kupitia mitandao yao ya kijamii huku likionesha furaha yao baada ya kumbeba gwiji huyo kutoka Amsterdam, Uholanzi hadi humu nchini.
Wafanyikazi wa shirika hilo walihakikisha kuwa wamepiga picha na bingwa huyo.
Waliandika,

Honoured to fly our CHAMPION

home from Amsterdam. The Pride is so proud of you!

Tazama picha zifuatazo.