kiunjuri

Picha za siku: Wakenya wamkejeli Mwangi Kiunjuri baada ya kupigwa kalamu

Hii leo, Mwangi Kiunjuri alifutwa kazi na rais Uhuru Kenyatta katika mabadiliko kwenye baraza la mawaziri yaliyotangazwa. Kiunjuri alikuwa waziri wa Kilimo naye Adan alikuwa waziri wa Jumuiya ya afrika Mashariki.

Raychel Omamo amehamishwa hadi katika wizara ya  Mashauri ya kigeni ilhali Sicily Kariuki amehamishwa hadi katika wizara ya Maji. Peter Munya sasa ndiye waziri mpya wa Kilimo ilhali Monica Juma amehamishwa hadi katika wizara ya Ulinzi.

Simon Chelegui amehamishwa kutoka wizara ya maji hadi ya leba ilhali  Ukur Yattani amethibitishwa kuwa waziri wa Fedha .

Kufutwa kwake kumejia baada yake kupigwa vita katika mitandao ya kijamii baada yake kusema wakenya wanapaswa kupiga picha nzige kisha wachapishe picha ili wizara ya kilimo ishughulikie janga hilo.

Hata hivyo wakenya walikimbia mitandaoni kumkejeli kwa masaibu yaliyomkumba.

Tazama picha zifuatazo.

kiu

kiu

kiu 2

 

Photo Credits: ezekiel Aming'a

Read More:

Comments

comments