(+PICHA)Dada yake Diamond Esma Platnumz afanya harusi ya pili ya kupendeza

Dada ya msanii wa bongo Diamond Platnumz, Esma Alhamisi usiku alifanya harusi ya kipekee na kupendeza, huku akiwa mke watatu wa mumewe.

Kupitia kwenye posti harusi hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa Esma na familia za pande zote mbili, pia baadhi ya wasanii wa lebo ya WCB walihudhuria miongoni mwa waliohudhuria ni Zuchu, Lavalava na Queen Darleen.

Huku akitangaza harusi yake Esma aliandika,

"Rafiki Zangu ,Vipenzi vyangu natamani wote tuwe pamoja tufurahi pamoja ila wengine majukumu mpo mbali basi tutakuwa tukifurahi na kushaherekea siku muhimu ya ndoa yangu na Mume wangu Kipenzi wa Halali .”

Ni hafla ilionyeshwa katika runinga ya Wasafi, inayomilikiwa na msanii Diamond na alikuwa na haya ya kusema,

"Kwanza niwaambie nina furaha kubwa sana kwa sababu namuozesha dadangu lakini furaha ya pili, kutokana na harusi ya dadangu name intanipa mtu wakunipenda name nimuoe.”

Hizi hapa baadhi ya picha za harusi hiyo.