(+PICHA)Msanii Zuchu atiririkwa na machozi baada ya kupatana na rais Magufuli ana kwa ana

Msanii wa lebo ya WCB Zuchu na mwanawe msanii mkongwe Khadija Kopa alibubujikwa na machozi Jumamosi baada ya kupatana na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ana kwa ana.

Zuchu alikuwa miongoni mwa wasanii waliohudhuria hafla ya chama cha CCM mjini Dodoma, aliwatumbuiza wanasaiasa na mashabiki mbele ya wanasiasa wa chama cha Mapinduzi(CCM).

Baada ya kuwatumbuiza wananchi na rais, Zuchu alienda kumsalimia Magufuli huku akitiririwa machozi kwa furaha aliokuwa nayo.

Msanii huyo kupitia kwenye mitandao ya kijamii aliandika haya baada ya hafla hiyo ya kukutana na Magufuli.

SUBIRA NI IBADA ALINAMBIA MAMAANGU.MATOKEA NDO NAYAONA SASA HIVI .LEO NA MIMI NATAMBULIKA KWA

MH:RAISI JOHN POMBE MAGUFULI. 😭😭MWENYEZI MUNGU ASANTE ASANTE KWA RAISI MWENYE UPENDO WA DHATI NA MWENYE KUTHAMINI KILA MTU. DREAMS DO COME TRUE NDO NAAMINI SASA.NAOMBA HII IWAGUSE WASCHANA WOTE AMBAO PENGINE HUJUI UTATOKA LINI MI NI SHAHIDI NAKWAMBIA PAMBANA SIKU YAKO INAKUJA .

MIEZI MITATU ILIYOPITA NINGEAMBIWA YATATOKEA HAYA NISINGEAMINI .

M/MUNGU ATUPE AFYA TUFIKE TAREHE 18/JULY TUWE WOTE MLIMANI CITY .KWENYE USIKU MAALUM WA KUWASHUKURU KWA SAPOTI HII. THIS IS UNFORGETTABLE." Zuchu Aliandika.

Msanii Diamond naye hakuwachwa nyuma na ambaye amekuwa akimsifia msanii Zuchu alikuwa na haya ya kunakili.

"RAIS MPENDA WATU, RAIS ANESIKILIZA NA KUWAJALI WANANCHI WAKE…..THANK YOU SO MUCH MR PREZIDENT…..@OFFICIALZUCHU USILIE, HIZO NI MBIVU ZA UVUMILIVU WAKO HADI SASA KUTAMBULISHWA…KUPITIA WEWE KUKAENDELEE KUWAPA THAMANI WANAAKE NA KUDHIHIRISHA KUWA WANAAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA….NAISUBIRIA KWA HAMU SIKU YAKO KUU PALE MLIMANI CITY HALL JUMAMOSI HII 🙏🏼 #IAMZUCHU #WCB4LIFE."