Polisi 5 wa akiba kuuwawa na mifugo kuibwa katika shambulizi Baringo

1898069(2)
1898069(2)
Maafisa 5 wa taifa wa akiba waliweza kuuwawa na idadi isiyo julikana ya mifugo kuibwa na majambazi ambao wanashukiwa walitoka Pokot, kisha kushambulia Arabal, Baringo Alhamisi asubuhi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Baringo Robinson Ndiwa alisema kisa hicho kilitendeka wakati ambao washambulizi hao waliweza kushika usukani nyumba za manyatta za Tugen na maafisa hao kuuwawa katika kisa hicho.

Maafisa 5 wa taifa wa akiba waliweza kuuwawa na idadi isiyo julikana ya mifugo kuibwa na majambazi ambao wanashukiwa walitoka Pokot kisha kushambulia Arabal, Baringo Alhamisi asubuhi.

"Tayari tushaaleta askari wa  GSU, RDU na NPR ili kuwatafuta wezi hao wa mifugo ambao wamepeleka mifugo hiyo maeneo ya, Tiasty East," Alisema Robinson.

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa wakazi hao wana wasiwasi na kuwauliza waweze kutulia kwa maana polisi wako katika kazi.

"Jambo hilo lili weza kufanya watu washangae na kushtuka kwa maana eneo hilo lilikuwa na amani, hakuna mtu yeyote aliweza kutarajia shambulizi hilo na wafugaji walikuwa wameacha mifugo wao wakule kwa huru," Ndiwa aliongea.

Mwanaharakati wa eneo hilo Ole'mpaka aliweza kuomba serikali waweze kutoa helikopta ili ziweze kutafuta wezi hao ambao waliweza kuiba mifugo.

Alisema kuwa wanaweza kuwa hawajaenda mbali, bali wamejificha vichakani.

"Maisha mengi yanaweza okolewa na kupata mifugo hao ambao waliibiwa kama watachukua hatua ya haraka," Alieleza Oli'mpaka.

Mbunge wa kaunti ya Baringo kusini Charles Kamuren aliuliza polisi wa ulinzi wafanye kazi kwa haraka ili kurudisha amani na kutuliza wakazi wa eneo hilo.

Aliweza kuwaambia wakazi wawe makini kwa maana washambulizi hao hawajulikani walienda njia gani na wako mbali wapi.

Mwaka jana September inasemekana kuwa maafisa wawili wa RDU na NPR waliweza kuumizwa na washambulizi waliokuwa wamejihami wa kutoka eneo la Pokot.

Katika kijiji cha Ramacha kata ndogo ya kaunti hiyo."Polisi hao walikuwa katika kazi yao kama kawaida ambapo majambazi hao waliweza kutokea na kupiga risasi hewani," Alieleza chifu wa eneo la Arabal William Koech.

Lakini ni lini wakazi hao watakaa na amani na lini wataacha kushambuliana wao kwa wao wenyewe.