Afisa wa polisi kushtakiwa kwa kumuua jamaa Mathare wakati wa kafyu

ZpQk9kpTURBXy8zMDg0ZjA0NjM4MWYxNDUwMzUzNDU5YjM2NDRmOGE0Mi5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
ZpQk9kpTURBXy8zMDg0ZjA0NjM4MWYxNDUwMzUzNDU5YjM2NDRmOGE0Mi5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Afisa wa polisi ameshtakiwa kwa mauaji ya jamaa mmoja katika mtaa wa Mathare mjini Nairobi kwa kumpiga risasi jamaa wakati wa saa za wa kutotoka nje.  Afisa huyo atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga.

Amri ya kutotoka nje iliwekwa  na rais Uhuru Kenyatta ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Vitalis Owino 36, aliaga dunia wiki jana na kupelekea maandamano ya wakaazi wakilalamikia mauaji yake.

Wakazi wa Mathare waliubeba mwili wa jamaa huyo na kuandamana hadi kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga wakitaka haki kutendeka.

Kulingana na mashahidi, Vitalis aliuawa na polisi eneo la Mathare Phase 4 walipokuwa wakishika doria eneo hilo.

Waandamanaji hao walitawanywa na polisi baada ya kuwasili eneo hilo na kuuchukua mwili huo.

Rais Uhuru Kenyatta amekuwa kila mara akiwataka maafisa wa polisi kuacha kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wananchi wanapotekeleza kafyu.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO