Polisi kuwazuilia mwanaume na mpenzi wake kwa kumuuwa mkewe

1886204
1886204
Polisi katika kaunti ya Kiambu wamepewa ruhusa na korti ya kaunti hiyo kwa kuwazuilia mwanaume na mpenzi wake kwa siku 14, kwa madai ya kwamba wamemuuwa mke wake.

Afisa wa uchunguzi Cornelius Arwaa ameiuliza korti kumpa siku zaidi za kumaliza uchunguzi juu ya kisa hicho.

Marehemu Mary Kamangara, 39, aliweza kuonekana kwa mara ya mwisho Jumamosi saa tano nyumbani kwake akienda kazini eneo la Kahawa Sukari ambapo amefungua duka la vifaa.

Kwanini mume wake akahusika katika mauaji ya mke wake na kwanini akakuwa na mpenzi wa kando ilhali ako kwenye ndoa?

Mwili wa mwendazake Mary uliweza kupatikana Jumapili katika kata ndogo ya Juja akiwa na majeraha ya kichwa.

Alikuwa na majeraha ya kina kichwani yaliyotolewa na kifaa butu na michibuko kwa upande wa mikono yake.

Polisi huyo alisema mume wa marehemu Joseph Kori Karue na mpenzi wake Judy Wambui Mungai ndio wahusika wakuu katika mauaji hayo.

Hii ni baada ya nguo zilizo kuwa na damu kupatikana chumbani mwa Judy alikoishi eneo la Four ways katika barabara ya Kiambu.

"Upasuaji bado haujafanywa ili kubaini kisa cha mauaji hayo na bado kurekodi kauli kutoka kwa mashahidi muhimu,na pia CCTV hazijaangaliwa katika hoteli ya Homeland na chumbani chake wambui cha fourways estate ambako Wambui na marehemu Polisi katika kaunti ya Kiambu wamepewa ruhusa na korti ya kaunti hiyo kwa kuwazuilia mwanaume na mpenzi wake kwa siku,14,kwawalitekwa na kamera hizo," Alieleza Cornelius.

Aliongezea na kusema nguo zilizo chukuliwa chumbani kwa Wambui zitafanyiwa DNA kwa uchunguzi zaidi.

Washukiwa hao wawili hawakuweza kuwakilishwa na wakili yeyote kwa hivo watakaa kituoni cha polisi cha Juja mpaka Februari 13.

Polisi mkuu wa kata ndogo ya Juja Simon Thirikwa alisema kuwa marehemu aliweza kuuwawa katika maeneo mengine na mwili wake kuja kutupwa katika eneo la hilo usiku wa manane.

Marehemu na mume wake waliishi eneo la Garden Estate home kaunti ya Nairobi. Kiio alisema kuwa bado wanafuatilia gari ya marehemu aina ya Mercedes C 200 Saloon na simu ya marehemu.

Ina maana kuwa mume wake na mpenzi wake wa kando walikuwa wamepanga jama hiyo au la?