Polisi Mombasa aponea baada ya kuchapwa na umati kwa kuwaambia wavae barakoa

mombasa
mombasa
Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Mombasa walizua vurugu, na kuanza kumchapa polisi mmoja kichapo cha mbwa hii ni baada ya kuwaambia wavae barakoa vyema kama vile wizara ya afya iliagiza.

Kikundi hicho kilisema kuwa polisi huyo alikuwa anawasumbua mbali na kuwaambia wavalie barakoa vyema.

Polisi huyo aliponea chupuchupu baada ya kupiga mayowe, yaliyosababisha wenzake kumsikia na kisha kuaj kumsaidia kutokana na kichapo cha wakazi hao.

Kupitia kwenye ripoti ilinakiliwa katika kituo cha polisi ilisema kuwa polisi huyo alipatwa na majeraha ya kichwa na mwili.

"The victim was rushed to Coast General Hospital and is in a stable condition."

Muuguzi kutoka hospitali hiyo alisema kuwa polisi huyo alipata majeraha ya kichwa bali anaendelea kupokea matibabu.

Hiki ni kisa cha awali ambacho polisi wanakabiliana na umati kwa kukaidi maagizo ya wizara ya afya, kisa cha Juni,6, wakazi wa kaunti ya Kisii walichoma kituo cha polisi cha Rioma kufuatia mauaji ya mwanabiashara wa eneo hilo huku wakidai kuwa polisi ndio walitekeleza kitendo hicho.

Ina maana kuwa wananchi wamechoka na vitendo ambavyo polisi wanawatendea au polisi wamechoshwa na ukaidi ambao wananchi wengi wanatekeleza licha ya kupewa maagizo na wizara ya afya?